Psalms 29

Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba

Zaburi ya Daudi.

1 aMpeni Bwana, enyi mashujaa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
2 bMpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
3 cSauti ya Bwana iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.

4 dSauti ya Bwana ina nguvu;
sauti ya Bwana ni tukufu.
5 eSauti ya Bwana huvunja mierezi;
Bwana huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.
6 fHufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni
Yaani Mlima Hermoni.
urukaruke kama mwana nyati.
7 hSauti ya Bwana hupiga kwa miali
ya umeme wa radi.
8 iSauti ya Bwana hutikisa jangwa;
Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
9 jSauti ya Bwana huzalisha ayala,
na huuacha msitu wazi.
Hekaluni mwake wote wasema,
“Utukufu!”

10 k Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;
Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
11 l Bwana huwapa watu wake nguvu;
Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.
Copyright information for SwhNEN